Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Bahjat amesimulia kumbukumbu aliyoinukuu kutoka kwa Ayatollah Sayyid Abdulhadi Shirazi kuhusu kuondoa umaskini, na tunaiwasilisha kama ifuatavyo.
Katika utoto wangu, baada ya kufariki baba yangu na Mirza mkubwa ambaye alikuwa akisimamia mambo yetu, jukumu la kulea familia liliangukia kwangu.
Nilimwona baba yangu katika ndoto.
Akaniuliza:
“Bwana Sayyid Abdulhadi! Vipi hali yako?”
Nikamjibu:
“Sio nzuri.”
Akasema: “Waambie watoto na watu wa nyumbani kwamba waswali swala mwanzo wa wakati, umaskini wenu utaondoshwa.”
Chanzo: Kituo cha "Sirah al-Ulama"
Maoni yako